Lango la Maji / Uvunaji wa Maji ya Mvua / K3 (Kutiliwa upya, Kuhifadhi, Kutumiwa upya)

From Akvopedia
Jump to: navigation, search
English Français Español भारत മലയാളം தமிழ் Swahili 한국어 中國 Indonesia Japanese

Kuna hoja tatu muhimu ziungazo K3:

1. Kufuatana na mabadiliko ya hali ya hewa
Mabadiliko katika kunyesha kwa mvua yanaweza kuathiri hali ilivyo ya kazi za watu pamoja na uwezo wao wa kiuchumi. Uhifadhi wa maji ni kipengele nyeti katika kuvumilia muda za ukame au tofauti baina ya upatikanaji na uhitaji wa maji. Ni afadhali kutumia maji ya chini ya ardhi, maji ya juu ya ardhi na mifumo ya uhifadhi maji. Mifumo hii inaweza kuwapatia watu maji ya kunywa pamoja na maji kwa ajili ya ngo’mbe, ukulima na mahitaji mengine ya ustawishi. Maji yananufaisha mazingira yakiwa ndani ya mfumo wa ikolojia. Kuhifadhi maji kunahakikisha kiasi kinachotosheza miuda ya ukame.

2. Kuyazungusha maji upya katika mlolongo wa maji
Usimamizi wa maji mara nyingi unakusudiwa kwa kielelezo cha mgawo wa maji, utaratibu na upatikanaji wake peke yake. Unakosa kuweka maanani kiasi kile kinachohitajika miuda ya ukame, uzungushaji wa maji ama utumiaji upya wa maji yaliyohifadhiwa. K3 inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko likiwa na uzuri wa maji ya rasilimali hifadhika. Kutumia na kutumia upya maji hifadhika kunaboresha upatikanaji wa maji kwa vile kunazuia migogoro kuhusu mgawo kwa kutumia na kutumia upya maji katika mlolongo wake.

3. Usimamizi wa maji yenye rangi ya majani
Kuhifadhi maji yaliyo juu ya ardhi kunaboresha unyevunyevu wa ardhi kukiongeza upatikanaji wa maji juu ya ardhi yaliyo na kina kifupi. Njia hii ya uhifadhi inachangia sana ‘usimamizi wa maji yenye rangi ya majani’. Usimamizi huu unakusudia unyevunyevu unaotokana na ulimaji bora, uwekaji matandazo, mifanyiko tendaji ya fiziokemikali pamoja na sayansi ya viumbe hai. Kutokana na kuingiza maji ardhini, K3 inachangia usimamizi wa maji yenye rangi ya majani kwa njia inayoweka taswira nzuri kwenye utoaji wa ukulima pamoja na mifumo ya ikolojia.

Kifaa cha Kupanga kwa K3

Katika programu za WASH, kuna lengo la akiba ya maji ya jamaa, elimusiha pamoja na udhibiti afya ambalo linakusudia familia au jumuiya hakuna likusudilo eneo au sehemu ya kuteka maji kama lilivyo katika Programu za Usimamizi wa Kufungamanisha Akiba za Maji. Hata hivyo programu za WASH zinazidi kuungana na sekta za vyakula na nishati. Kufanya hivyo kunaleta kufikiria upya programu za WASH pamoja na kuelekea kutoka kwa programu ya jumuiya hadi programu yanayokusudia sehemu ya kuteka maji.

Kutokana na ongezeko la mahitaji ya maji yakiwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, ni muhimu mno kuhifadhi maji kwa uangalifu katika sehemu ya kuteka maji. Mpango wa K3 (yaani kutiliwa upya nguvu, kuhifadhi na kutumiwa upya) zaidi ya kuboresha usimamizi wa akiba ya maji na chakula katika sehemu ya kuteka maji kusudi la ulinzi lakini unaunga mkono majumuiya kufanya kazi pamoja wakikabidhiwa na uhaba wa maji pamoja na kusimamia vitu vya lazima vilivyopondani ya sehemu ya kuteka maji. Hata hivyo changamoto ipo katika kufungamanisha mpango wa K3 katika mipango na utekelezaji wa mipango katika majumuiya.

Matakwa na Mipaka

Kifaa hiki cha kupanga kinalenga miradi inayofanyika na ubia wa K3 nchini Ethiopia na Nepal. Ingawaje lengo ni kukuza kifaa cha kupanga ambacho kinatumika katika muktadha mbalimbali, haiwezekani kitumike moja kwa moja kile kinnachokusudia Ethiopia na Nepal kwa nchi nyingine pasi na mabadiliko faafu. Kifaa hiki kinakusudiwa kwa watu wa serikali pamoja na wale wa taasisi za usimamizi wa maji na mipango ya matumizi ya nafasi.

Maelezo na matokeo

Mnamo mwaka wa 2012 nchini Nepal, RAIN pamoja na Acacia Water zilianzia mradi wa K3 unaounga mkono ushiriki wa maji kufungamanisha mfumo wa K3 katika mipango ya miradi yao. Mfumo huu unazaa fursa pamoja na changamoto sehemu fulani zitakazokuwepo kwa kutazama mazingira ya maumbile hai pamoja na mazingira ya kijamii. Mnamo mwaka wa 2012 MetaMeta pamoja na RAIN zilifanya kazi za kujenga uwezo wa serikali za majumuiya kutekeleza malengo ya K3 yakiwa sehemu ya mfumo uliopo wa usimamizi wa maliasili. Miradi yote miwili ilidhihirisha haja ya K3 kama kifaa cha kupangia miradi ya usimamizi wa matumizi ya maji. Isitoshe, akili, uwezo na wajibu zinahitajika ili kubadilisha milolongo iliyopo ya upangaji wa mashirika ya kiserikali pamoja na yale yasiyo ya kiserikali.

Kifaa cha Kukadiria Sehemu ya Kuteka Maji

RAIN pamoja na Practica Foundation na Wetlands International zitakuza kifaa cha kukadiria sehemu ya kuteka maji kitakachohimili miradi ya WASH ambayo kitafanya kazi na mwelekeo uendeshwao na eneo (badala ya ule uendeshwao na teknolojia.) Vipo vifaa vingi vya aina hii lakini kwa kawaida vifaa hivi vinatatiza matumizi kwa kutoelekeza kwa urahisi, kwa hivyo havifai mipango midogo ya miradi ya UMM. Kifaa hiki kimetokana na kifaa kingine cha RAIN ambacho kinahimili uamuzi nacho bado kinakuzwa kikiwa na vifaa vingine vya aina hii ambavyo vimeshachangia ukuzaji wa kifaa hiki kipya.

Matakwa na Mipaka

Kifaa hiki kipya kinaweza kutumika katika matumizi ya mipango midogo ya sehemu za kuteka maji yakikusudia maeneo yenye ukavu au ukame. Kifaa hiki kinakuzwa kutumiwa na wafanya kazi na wasimamizi wa programu za WASH waliopo nchi zinazoendelea.

Maelezo na Matokeo

Kifaa hiki kikusudiwacho kinahimili mipango ya WASH inayojiingiza mapema katika mipango ya suluhu ya hali za ukavu na ukame. Pia, kinakadiri fursa zikiwa na hatari zilizopo katika eneo kusudiwa au sehemu ya kuteka maji. Kinajenga njia zenye kulinda mazingira pamoja na na kuunga mkono uamuzi zenye busara za programu za WASH.

Uhimili wa Uamuzi wa UMM: Uvunaji wa Maji ya Mvua

Mnamo mwaka wa 2010, kifaa cha uhimili wa uamuzi wa UMM kilitengenezwa na RAIN kilichomo katika mazingira ya Wiki. Lengo la mradi huu lillikuwa kukuza kifaa cha kupangia na kukata shauri katika kuongoza utekelezaji, uboreshaji na ufungamanisho wa UMM katika programu za usimamizi wa maji. Mkakati wake ni hatua 14 ambazo zitamwongoza mtumiaji akielekea katika vipengele tofauti vya uvunaji wa maji ya mvua. Kifaa hicho kinaungana na maktaba yenye maarifa zaidi kuhusu vipengele vya uvunaji wa maji. Mifano ni pamoja na masuala ya uzuri wa maji lakini pia maarifa juu ya vitendo faafu vya uvunaji wa maji. Maarifa zaidi yanapatikana katika ripoti ya mwisho.

Maelezo & matokeo

Kifaa hakijachapishwa/dhibitiwa na tarakilishi kuu, sababu maalum ya kutofanya ni kuonekana kutoelezeka kwa urahisi (kina hatua 14) kwa hivyo kuwa kigumu na chenye kutwisha akili ya mtumiaji. Lengo la RAIN sasa hivi ni kutengeneza upya kifaa kiwe kitumike kwa urahisi zaidi kikamfurahisha mtumiaji. Kifaa hichi kipya kiko njiani kinakuja.

Matokeo ya matumizi ya K3

Miradi ifuatayo inatumia K3 kwa kutiliwa nguvu upya, kuhifadhiwa, na kutumiwa upya.

Akvorsr logo lite.png
Mradi wa RSR 394
Kujulisha K3 katika eneo likusudiwalo la DWA
Mradi wa RSR 427
Upimaji wa Njia ya Upataji Maji
Mradi wa RSR 572
Kujulisha K3 kwa eneo likusudiwalo katika DWA

Nyaraka, video, na viungo