Lango la Maji / Uvunaji wa Maji ya Mvua / Ukuzaji wa Biashara - Jinsi ya Kugharimia Biashara

From Akvopedia
Jump to: navigation, search
English Français Español भारत മലയാളം தமிழ் Swahili 한국어 中國 Indonesia Japanese Russian
Mkulima wa Nepal alijenga tangi lake la uvunaji wa maji ya mvua kwa mkopo uliogharimiwa na kitega uchumi kidogo. Foto: RAIN document.

Uvunaji wa maji ya mvua umetangazwa kuwa uchaguzi badili kwa kupata akiba ya maji, bali pia umetangazwa kutofaa. Sababu kuu katika kukosoa ni bei yake kuwa ghali hasa kwa wanavijiji masikini. Uwekezaji wa kimsingi unaleta bei ya juu kutokana na kutokuwa na kitovu cha utendaji pamoja na akiba ndogo ya maji. Hata hivyo kwa kutazama gharama za mzunguko wa maisha (GMM) ya tangi, wazo hili halionekani kuwa na shida. Kwa mfano matangi ya maji ya mvua kwa wastani, yana maisha ya miaka 20. Pia uvunaji wa maji ya mvua huenda yanaleta mapato, elimu bora na upungufu wa matatizo ya afya. Lakini nani anaweza akiwa tayari kulipia gharama za uwekezaji wa kimsingi ijapokuwa kuna uthibitisho wa kuwa bei ya GMM ni chini zaidi huku kitega uchumi hiki kitaleta faida?

Matakwa na mipaka

Makala hii inaeleza ujuzi za RAIN katika kupata uwekezaji wa kudumu kwa miradi ya uvunaji wa maji ya mvua iliyofanyika nchini Senegali, Bukinafaso na Nepali. Itatafakari ujuzi hizi na kuzilinganisha na utafiti na utendaji wengine wa uvunaji wa maji ya mvua, vitega uchumi na ukuzaji wa biashara nyingine. Shirika zisizo na uhusiano na serikali zikiwa pamoja na watumiaji wengine wa miradi hiyo watajifunza fursa pamoja na changamoto zilizopo katika kubadilisha muundo wa kiuchumi wa programu za maji ya mvua.

Maelezo & matokeo

Miradi mitatu ya majaribio imetekelezwa nchini Nepali tangu mwaka wa 2010. Nayo inahusika na ukopeshaji wa pesa zikusudiwazo na miradi ya uvunaji wa maji ya mvua. Uchunguzi wa uwezekano yakinifu wa kuweza kuwepo kwa vitega uchumi nchini Bukinafaso na Senegali umetendewa. Huko Nepali, shirika la BSP-Nepal likiwa na ubia na RAIN limetekeleza shabaha ya kupunguza kiasi cha ruzuku kwa 25% ambacho sasa ni mkopo mdogo. Mikopo sasa hulipiwa huku matokeo ya kimsingi yanaelekea kuwa afadhali. Mnamo mwaka wa 2012 WASTE ilifanya tathmini iliyobainisha ya kuwa vitega uchumi vidogo vya mifumo ya uvunaji wa maji ya mvua vinaleta faida. Isitoshe mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha VU, Amsterdam anayetimiza shahada ya uzamili amefanya utafiti yakinifu kuhusu mikopo ihusikayo na uvunaji wa maji ya mvua nchini Nepali.

Mifano

Nyaraka, video, na viungo

RAIN and BSP-Nepal : working together in rainwater harvesting in Nepal.